Mengineyo
 
 
 


KUHUSU TPC

Historia
MARA tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa vyama vingi nchini mwaka 1995, Chama cha Waandishi wa Habari na Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari (AJM) kilichokuwa kikishughulikia taarifa zilizotolewa wakati wa uchaguzi, kilipata wazo la kuanzisha Kituo cha Habari, ambacho kingeshughulikia udhaifu wa kitaaluma unaooneshwa na waandishi wa habari pamoja na wale wasio katika fani hiyo.

Bahati njema, Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari (IFJ) likakubali kusaidia kuanzishwa kwa Kituo cha Habari Tanzania (TPC), kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya.

Tangu wakati huo, TPC imeshiriki katika miradi mbalimbali, ikishirikiana na AJM, ambayo kwa njia moja au nyingine ilisaidia kuwaongezea
ujuzi wa kitaaluma waandishi wa habari na kupigania ustawi wao na haki zao za kikazi.

Mafanikio pekee makubwa ya TPC mwaka 2001 yalikuwa ni kuwezesha kuanzishwa kwa chama cha wafanyakazi katika sekta ya habari.
Chama hiki kinafahamika kama Tanzanian Union of Journalists (TUJ) na kilianzishwa kwa lengo la kupigania haki za kikazi za waandishi
wa habari, pamoja na kuwaendeleza waandishi wa habari kitaaluma.

TPC pia ilikuwa chachu na ilisaidia katika jitihada za kuanzishwa kwa Baraza la Habari Tanzania.

Tamko la Maarubu
TPC ni chombo cha kupigania maendeleo ya sekta ya habari na taaluma ya habari, kwa njia ya kuwezesha watu binafsi na taasisi, hapa
nchini na kimataifa.

TPC inavyotekeleza majukumu yake:
Mafunzo ya muda mfupi kwa wahariri na waandishi TPC huendesha mafunzo ya muda mfupi katika maeneo ya uhariri, misingi ya uandishi wa habari, uandishi wa habari za uchunguzi, uandishi wa masuala maalumu (mfano uandishi wa habari za kibiashara, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia), upigaji picha, uchoraji katuni na michoro, matumizi ya kompyuta katika uandishi wa habari na kadhalika.

Kuanzia Mei 2004, TPC iliongeza nguvu zake katika kusaidia vyombo vya habari vya Kiswahili na vya kijamii nchini Tanzania.

Kwa msaada wa hisani kutoka Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD), TPC inashirikiana na Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na African Virtual University (AVU) kuunda istilahi za Kiswahili (zipatazo 650,000) kwa ajili ya kuanzisha toleo la Kiswahili la Microsoft Windows na Office ifikapo 2005.

TPC iko mstari wa mbele kuona Watanzania wanawezeshwa kutumia kompyuta na mitandao ya ndani na nje kwa Kiswahili.

Hili tunaamini litawezesha Watanzania walio wengi zaidi kunufaika na maendeleo ya TEKNOHAMA duniani.

Wakati huo huo, TPC inashirikiana na wakufunzi na walimu katika vyuo vya Uandishi wa habari nchini na wafanyakazi wa vyombo vya habari wenye taaluma ya uandishi wa habari pamoja na wadau wengine, kutengeneza vitabu vya kufundishia maeneo mbalimbali ya
taaluma ya uandishi, elimu na maarifa mengine kwa Kiswahili - mradi wenye lengo la kuinua ubora na viwango vya waandishi pamoja na
wafanyakazi wengine wa vyombo vya habari vya Kiswahili.

Msaada kwa waandishi wa kujitegemea
Takriban asilimia 80 ya waandishi wa habari wanaofanya kazi katika magazeti na vyombo vya habari vya eletroniki nchini Tanzania si
wenye ajira za kudumu katika kampuni wanazofanyia kazi.

Kituo kimedhamiria kuwasaidia waandishi wa habari wa kujitegemea nchini na ndicho kilichowezesha kuanzishwa kwa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kujitegemea nchini (FREJAT).

Hata hivyo, uhaba wa vifaa, mathalani kompyuta za kufundishia masomo ya kompyuta na ujuzi wa barua-pepe na tovuti hukwamisha
jitihada zetu za kuwasaidia waandishi wa habari wa kujitegemea.

Ushirikiano na asasi za kibiashara na taasisi
Mikutano inayofanyika mara kwa mara baina ya waandishi wa habari na asasi za kibiashara au taasisi za umma kama vile polisi,
husaidia kuifanya kazi ya waandishi wa habari na maisha yao kuwa rahisi zaidi.

Mikutano ya aina hiyo pia husaidia kupanua uelewa wa waandishi wa habari wengi, kuhusiana na mazingira ya kazi ya asasi na taasisi hizo husika.

Msaada kwa Klabu za Habari
TPC, kwa kushirikiana na klabu za waandishi wa habari za Mbeya, Ruvuma na Rukwa na kwa msaada wa kampuni ya Business Times
Limited ilishiriki kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa maeneo husika katika warsha mbalimbali zilizofanyika kati ya mwaka 1999
na 2001.

Klabu za waandishi wa habari za Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Chama cha Waandishi wa Habari cha Zanzibar (JAZ) zilinufaika na
programu za mafunzo za aina hiyo zilizofanyika kati ya 2001 na 2002. Mikoa iliyonufaika ni asilimia 30 ya mikoa yote ya Tanzania.

Klabu zipatazo 17 za waandishi wa habari pia zimeona umuhimu wa kuwa na mafunzo kama haya, ambayo huwezesha kuanzishwa
kwa magazeti ya jamii katika maeneo husika.

Uhaba wa fedha umekwamisha jitihada za kupanua programu ya mafunzo kwa waandishi
wa habari wa mikoani wasio na taaluma ya uandishi wa habari na kwa kiasi kikubwa wametengwa, kwani programu nyingi hupendelea zaidi Dar es Salaam na miji mingine mikubwa hapa nchini.

UZINGATIAJI WA TAALUMA
Kwa njia ya:
Kuimarisha vyombo vya habari vya Kiswahili Afrika Mashariki na Kati kuzalisha na kuanzisha software/programu muafaka za kompyuta kwa ajili ya vyombo vya habari na kadhalika kuhimiza matumizi ya TEKNOHAMA katika vyombo vya habari
Kutoa mafunzo ya uandishi wa habari, uhariri, utengenezaji kurasa na uzalishaji, uongozi, TEKNOHAMA na lugha.

Kutoa mafunzo kwa ajili ya kuongeza ujasiliamali, sanaa, ubunifu na ujuzi katika fani ya uandishi mafunzo maalumu na mitandao shirikishi kufanya shughuli za ushauri, utafiti na maendeleo kwa ajili ya vyombo vya habari na kadhalika.

Kutoa msaada kwa waandishi wa habari wa kujitegemea kushirikiana na kujenga madaraja kati ya vyombo vya habari na asasi za kibiashara.

Kushirikiana na, na kuzisaidia klabu za waandishi wa habarizinazotumia Kiswahili popote pale duniani kusaidia kutoa mafunzo kwa vyombo vya habari vya kijamii-na hasa vile vya shule, vyuo, sehemu za kazi, kata, kijiji, tarafa, wilaya, mkoa na kadhalika.

Mazungumzo na mihadhara kutoka kwa wataalamu kujishirikisha na wafanyakazi wa vyombo vya habari ubia na vyombo vya habari vya jamii
UENDESHAJI

Anwani:
TANZANIA PRESS CENTER
Manzese Tip Top,
Usangi House, Ghorofa ya 3,
S.L.P. 11337,
Dar es Salaam,
TANZANIA.
Barue-e: tpc2003@journalist.com


WAHUSIKA:
Barua-e:
vevalist@yahoo.com
mayugwa@yahoo.com
sammy.makilla@journalist.com


Kupromoti Vyombo vya Habari vya Kijamii
TPC sasa ina mwelekeo pia wa kujizatiti katika kusaidiakuanzishwa kwa vyombo vya habari vya jamii nchini.

Jaribio letu la kwanza lilianza kwa kishindo mwaka 2001, kwa kuanzishwa kwa gazeti la kijamii la Nyasa, lililokuwa linatoka mara moja
kwa juma kwa ajili ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Klabu ya Starehe ya TPC
Mwaka 2005, TPC inapanga kuanzisha Klabu ya Starehe ya Jioni, ambapo waandishi wa habari na familia zao watakutana na kusikiliza
mihadhara juu ya mada mbalimbali; muziki, sanaa za maonesho na mihadhara mingine ya kisanaa na burudani, kinywaji na starehe kwa
ujumla.

Tunatafuta msaada kutoka taasisi mbalimbali za kibiashara hapa nchini, kwa ajili ya kuhakikisha mradi huu unafanikiwa.|

Kituo cha Habari Tanzania (TPC)
Kuelekea katika matumizi halisi ya taaluma kupitia mafunzo ya vitendo na ya muda wote
Imani iliyojengwa kwenye menejimenti nzuri na ya uhakika na matumizi ya Kiswahili kwa ajili ya kuongeza ubora wa maisha ya kazini ya
waandishi wa habari na jamii ya Watanzania kwa ujumla.

Habari na Matukio
 
Tovuti ya TPC sasa iko hewani!
 
Jinsi ya kuongea Kiswahili fasaha
©2004 Tanzania Press Centre. Haki zote zimehifadhiwa.